JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA

Huduma

Maendeleo Binafsi

Afisa yeyote bila kujali taaluma yake, atalazimika kuhudhuria mafunzo mbalimbali ya uongozi kwa kuzingatia cheo alichonacho. Mafunzo hayo yanaweza kuendeshwa kufuata taaluma au yakawa kwa pamoja. Kufaulu mafunzo hayo, kutakuwa ni sharti mojawapo katika kupandishwa cheo. 
Mafunzo hayo ni kama ifuatavyo: 

Uongozi wa Patuni. 
Mafunzo hayo yanawahusisha maafisa wenye cheo cha 
Luteni. Taaluma mbalimbali zinaweza kuendesha 
mafunzo yanayolingana na hayo, kwa mfano: Signal 
Platoon Commander, Kozi ya Ugavi na utuzaji mali 
(Logistic & Stores), Officers Basic Gunnery, Sub 
Lieutenant Technical, Air Defence Platoon Commander.

Uongozi wa Kombania. 
Mafunzo hayo yanawahusisha maafisa wenye cheo cha Kapteni. Maafisa wa taaluma mbalimbali wanaweza kufanya mafunzo yanayolingana na hayo kwa mujibu wa fani zao. (Logistic Company Commander, Specialization (Navy), Signal Company Commander na Air Defence Company Commander). 

Mafunzo ya Unadhimu na Ukamanda mdogo. (Junior Command and Staff Course). Mafunzo hayo yanahusisha maafisa wa kamandi zote wenye vyeo vya Kapteni. 

Mafunzo ya Unadhimu na Ukamanda. (Senior Command and Staff Course). Mafunzo hayo yanahusisha maafisa wa kamandi zote wenye vyeo vya Meja. 

Management Course. Mafunzo hayo yahahusisha maafisa wa fani zote wenye cheo cha Meja ambao hawakupitia Command and Staff Course. 

Unit Commanders Course. Maafisa wakuu watakaotarajiwa kupewa madaraka ya Kamanda Vikosi. 

High Commanders Defence Studies. Mafunzo hayo yanahusisha maafisa wa fani zote wenye cheo cha Luteni Kanali. 

National Defence College and War College Course. Mafunzo hayo yanahusisha maafisa wa fani zote wenye vyeo vya kanali na kuendelea. 

Mafunzo ya awali 

 • Askari aliyeandikishwa Jeshi atafanya mafunzo ya awali ya Kijeshi. 
 • Atahamishiwa kwenye kikosi ambacho atapangiwa kazi na ataendelea kufanya mafunzo. 

  Kozi za Ujuzi 
 • Atafanya kozi za ujuzi kwenye kikosi chake kwa kufuata mtiririko wa ngazi za ujuzi toka ngazi ya chini kwenda ngazi ya juu katika taaluma yake.
 • Kufaulu kozi kutakuwa moja ya masharti katika kufikiriwa kupandishwa cheo katika taaluma toka L-3 hadi Master level.
 • Kozi za ujuzi zinaweza kufanyika ndani au nje ya Jeshi

Mafunzo Ndani ya Jeshi 

 • Yatahusu kozi zile ambazo ujuzi wake hutolewa Jeshini.
 • Yatachukuliwa baada ya askari wapya kufika kwenye Vikosi vyao.
 • Yanaweza kuendeshwa kwa askari wa kiume na wa kike kwa pamoja au yanaweza yakatenganishwa kulingana na mazingira ya wakati huo.

Mafunzo ya Uongozi 
-Askari yeyote bila kujali taaluma yake atapaswa kufanya kozi mbali mbali za uongozi kulingana na cheo chake. 
-Kufaulu kozi hizo kutakuwa sharti mojawapo katika kufikiriwa kupandishwa cheo.Kozi hizo ni:- 

 • Junior NCOs Course pamoja na kozi ya ukufunzi kwa Praveti na Koplo.
 • Senior NCOs Course pamoja na kozi ya ukufunzi kwa sajini.
 • Warrant Offrs Course kwa WO2.
 • Regimental Sergeant major Course kwa WO1.
 • Management Course kwa WO1.

Kozi Nje ya Jeshi 

 • Maafisa na askari wanapewa nafasi ya kuhudhuria kozi za taaluma mbalimbali zinazoendeshwa katika vyuo nje ya Jeshi. Kozi hizo ni zile zenye manufaa kwa Jeshi. (Wahandisi, Wahasibu, Waganga, Wanamaji, Waongoza Ndege n.k).
 • Kozi hizo zinaweza kuchukuliwa ndani au nje ya Tanzania.